Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Hesabu 24:19 - Swahili Revised Union Version Mwenye kutawala atakuja kutoka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.” Biblia Habari Njema - BHND Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mmoja wa wazawa wa Yakobo atatawala naye atawaangamiza watakaonusurika wa Ari.” Neno: Bibilia Takatifu Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo na kuangamiza walionusurika katika mji.” Neno: Maandiko Matakatifu Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo na kuangamiza walionusurika katika mji.” BIBLIA KISWAHILI Mwenye kutawala atakuja kutoka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini. |
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa makabila ya watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.
Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.
Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.
Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atapata uharibifu.
Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
Lakini kuhusu Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
Naye yuko katika mkono wa kulia wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.