Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 24:18 - Swahili Revised Union Version

Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Edomu itamilikiwa naye, Seiri itakuwa mali yake, Israeli itapata ushindi mkubwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Edomu itamilikiwa naye, Seiri itakuwa mali yake, Israeli itapata ushindi mkubwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Edomu itamilikiwa naye, Seiri itakuwa mali yake, Israeli itapata ushindi mkubwa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Edomu itamilikiwa, Seiri, adui yake, itamilikiwa, lakini Israeli atakuwa na nguvu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Edomu itamilikiwa, Seiri, adui wake, itamilikiwa, lakini Israeli atakuwa na nguvu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 24:18
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Alaaniwe yeyote yule atakayekulaani, Na abarikiwe yeyote yule atakayekubariki.


Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.


Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.


Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi ushindi kila kokote alikokwenda.


Ndipo BWANA akamwinulia Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; aliyekuwa wa wazawa wake mfalme wa Edomu.


Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu,


Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena.


Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni; tazama, utashukia Edomu, na juu ya watu wa laana yangu, ili kuwahukumu. Oba 1-14; Mal 1:2-5


Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.


Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;


wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema BWANA, afanyaye hayo.


Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.


Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga.


Mwenye kutawala atakuja kutoka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini.