Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezra 1:9 - Swahili Revised Union Version

Na hii ndiyo hesabu yake; sinia za dhahabu thelathini, sinia za fedha elfu moja, visu ishirini na tisa;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ifuatayo ndiyo hesabu yake: Bakuli 30 za dhahabu; bakuli 1,000 za fedha; vyetezo 29;

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ifuatayo ndiyo hesabu yake: Bakuli 30 za dhahabu; bakuli 1,000 za fedha; vyetezo 29;

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ifuatayo ndiyo hesabu yake: bakuli 30 za dhahabu; bakuli 1,000 za fedha; vyetezo 29;

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hii ilikuwa orodha ya vifaa: masinia ya dhahabu yalikuwa thelathini; masinia ya fedha yalikuwa elfu moja; vyetezo vya fedha vilikuwa ishirini na tisa;

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na hii ndiyo hesabu yake; sinia za dhahabu thelathini, sinia za fedha elfu moja, visu ishirini na tisa;

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezra 1:9
14 Marejeleo ya Msalaba  

na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu.


Na vyetezo, na mabakuli; vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.


Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.


Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;


Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu.


mabakuli ya dhahabu thelathini, mabakuli ya fedha ya namna ya pili mia nne na kumi, na vyombo vingine elfu moja.


nami nikawapimia mikononi mwao talanta za fedha mia sita na hamsini na vyombo vya fedha talanta mia moja; na talanta mia moja za dhahabu;


na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu moja; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong'aa, thamani yake sawa na dhahabu.


Hivyo makuhani na Walawi wakaupokea uzani wa fedha, na dhahabu, na vyombo, ili kuvileta Yerusalemu nyumbani kwa Mungu wetu.


na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga;


Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.