Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme.
Danieli 2:49 - Swahili Revised Union Version Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya utawala wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akikaa katika lango la mfalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Danieli akamwomba mfalme, naye mfalme akawaweka Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya mkoa wa Babuloni. Lakini Danieli akabakia katika jumba la mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Danieli akamwomba mfalme, naye mfalme akawaweka Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya mkoa wa Babuloni. Lakini Danieli akabakia katika jumba la mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Danieli akamwomba mfalme, naye mfalme akawaweka Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa mambo ya utawala ya mkoa wa Babuloni. Lakini Danieli akabakia katika jumba la mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme. Neno: Maandiko Matakatifu Zaidi ya hayo, kwa ombi la Danieli, mfalme akawateua Shadraki, Meshaki na Abednego kuwa wasimamizi wa jimbo la Babeli, huku Danieli akibaki katika ukumbi wa mfalme. Swahili Roehl Bible 1937 Danieli alipomwomba mfalme, akawaagizia akina Sadiraki na Mesaki na Abedi-Nego kazi ya kuliangalia jimbo la Babeli, naye Danieli akakaa jumbani mwa mfalme. |
Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme.
Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili kati ya matowashi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, waliolinda milango ya vyumba vya mfalme, walikasirika sana, wakataka kumwua mfalme Ahasuero.
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
wakuu wote wa mfalme wa Babeli wakaingia, wakaketi katika lango la katikati, yaani, Nergal-Shareza, mnyweshaji, Nebu-Sarseki, mkuu wa matowashi, Nergal-Shareza, mkuu wa wanajimu, pamoja na wakuu wengine wote wa mfalme wa Babeli.
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.
Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake;
Nebukadneza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.
na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili wakuu hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara.
Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba BWANA, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.