Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.
Danieli 11:9 - Swahili Revised Union Version Naye huyo ataingia katika ufalme wa mfalme wa kusini, lakini atarudi mpaka nchi yake mwenyewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini baadaye, mfalme huyu wa kaskazini atauvamia ufalme wa kusini, ila atalazimika kurudi katika nchi yake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini baadaye, mfalme huyu wa kaskazini atauvamia ufalme wa kusini, ila atalazimika kurudi katika nchi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini baadaye, mfalme huyu wa kaskazini atauvamia ufalme wa kusini, ila atalazimika kurudi katika nchi yake. Neno: Bibilia Takatifu Kisha mfalme wa Kaskazini atashambulia nchi ya mfalme wa Kusini, lakini atarudi hadi kwenye nchi yake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha mfalme wa Kaskazini atashambulia nchi ya mfalme wa Kusini, lakini atarudi nyuma hadi kwenye nchi yake. Swahili Roehl Bible 1937 Lakini yule atakuja, auingie ufalme wa mfalme wa kusini, kisha atarudi katika nchi yake. |
Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.
Na mfalme wa kusini ataingiliwa na ghadhabu, naye atatoka na kupigana naye, yaani, na mfalme wa kaskazini; naye atapanga jeshi kubwa; na jeshi hilo litawekwa mikononi mwake.
Na mfalme wa kusini atakuwa na nguvu; lakini mmoja wa maofisa wake atakuwa na nguvu zaidi kuliko yeye, na atatawala; himaya kubwa zaidi kuliko yeye.
na miungu yao, pamoja na sanamu zao, na vyombo vyao vizuri vya fedha na dhahabu atavichukua mpaka Misri; kisha atajizuia miaka kadhaa asimwendee mfalme wa kaskazini.
Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wanatoka kwenda katika nchi ya magharibi; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hadi nchi ya kusini.
Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.