Amosi 8:7 - Swahili Revised Union Version BWANA ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu ameapa kwake mwenyewe, aliye Fahari ya Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. Neno: Maandiko Matakatifu bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. BIBLIA KISWAHILI BWANA ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo. |
Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! BWANA hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?
Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.
Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.
Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.
Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana.
Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.