Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Amosi 8:7 - Swahili Revised Union Version

7 BWANA ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mwenyezi-Mungu, fahari ya Yakobo, ameapa: “Hakika, sitayasahau matendo yao maovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mwenyezi Mungu ameapa kwake mwenyewe, aliye Fahari ya Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 BWANA ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo.

Tazama sura Nakili




Amosi 8:7
19 Marejeleo ya Msalaba  

Huwapa usalama, nao wapumzika kwao; Na macho yake yako juu ya njia zao.


Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe.


Ametuchagulia urithi wetu, Fahari ya Yakobo ampendaye.


Mungu amepaa kwa kelele za shangwe, BWANA kwa sauti ya baragumu.


Mhesabieni Mungu nguvu; Enzi yake imo juu ya Israeli; Na nguvu zake ziko mawinguni.


akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.


Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;


Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.


Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! BWANA hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake?


Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.


Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.


Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.


Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana.


Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.


Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo