Kwa sababu nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba;
Amosi 6:12 - Swahili Revised Union Version Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu. Biblia Habari Njema - BHND Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu. Neno: Bibilia Takatifu Je, farasi wanaweza kukimbia kwenye miamba iliyochongoka? Je, mtu aweza kulima kwa maksai huko? Lakini mmegeuza haki kuwa sumu na matunda ya uadilifu kuwa uchungu: Neno: Maandiko Matakatifu Je, farasi waweza kukimbia kwenye miamba mikali? Je, aweza mtu kulima huko kwa maksai? Lakini mmegeuza haki kuwa sumu na matunda ya uadilifu kuwa uchungu: BIBLIA KISWAHILI Je! Farasi watapiga mbio juu ya mwamba? Je! Mtu atalima kwa plau na ng'ombe baharini? Hata mmegeuza hukumu kuwa sumu, na matunda ya haki kuwa uchungu; |
Kwa sababu nilijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba;
Ee BWANA, macho yako je! Hayaangalii uaminifu? Umewapiga, lakini hawakuhuzunika; umewakomesha, lakini wamekataa kurudiwa wamefanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba wamekataa kurudi.
Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.
Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.
nami nitamkatilia mbali mwamuzi atoke kati yake, nami nitawaua wakuu wake pamoja naye, asema BWANA.
Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.
Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.