Amosi 5:8 - Swahili Revised Union Version mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Biblia Habari Njema - BHND Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni, ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana, na mchana kuwa usiku; yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi kavu, Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake. Neno: Bibilia Takatifu (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya nchi: Mwenyezi Mungu ndilo jina lake; Neno: Maandiko Matakatifu (yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni, ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko na mchana kuwa usiku, ambaye huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: bwana ndilo jina lake; BIBLIA KISWAHILI mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake; |
Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini.
Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.
Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.
Basi, tazama, nitawajulisha, mara moja hii nitawajulisha, mkono wangu, na nguvu zangu; nao watajua ya kuwa, jina langu ni YEHOVA.
BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi,
Kwa maana, angalia, yeye aifanyaye milima, na kuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; BWANA, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.
Tena itakuwa siku hiyo, asema Bwana MUNGU, nitalifanya jua litue wakati wa adhuhuri, nami nitaitia nchi giza wakati wa nuru ya mchana.
Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.
Watu wale waliokaa katika giza Wameona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti Mwanga umewazukia.
Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.