Musa akasema, BWANA asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri;
Amosi 5:17 - Swahili Revised Union Version Tena katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwako kulia; kwa maana mimi nitapita katikati yako, asema BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu; maana nitapita kati yenu kuwaadhibu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu; maana nitapita kati yenu kuwaadhibu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu; maana nitapita kati yenu kuwaadhibu. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Kutakuwa na kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, kwa kuwa nitapita kati yenu,” asema Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kutakuwepo kuomboleza katika mashamba yote ya mizabibu, kwa kuwa nitapita katikati yenu,” asema bwana. BIBLIA KISWAHILI Tena katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwako kulia; kwa maana mimi nitapita katikati yako, asema BWANA. |
Musa akasema, BWANA asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri;
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mharibifu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Furaha na shangwe zimeondoshwa, katika shamba lizaalo sana, na katika nchi ya Moabu; nami nimeikomesha divai katika mashinikizo; hapana mtu atakayekanyaga zabibu kwa shangwe; shangwe ile itakuwa si shangwe.
Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, nikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.
Nami nitapiga kambi yangu pande zote za nyumba yangu ili kuwapinga adui, mtu awaye yote asipite ndani yake wala kurudi; wala mtu aoneaye hatapita tena kati yao; kwa maana sasa nimeona kwa macho yangu.