Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 1:12 - Swahili Revised Union Version

12 BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake: “Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu, wao wataangushwa na kuangamizwa. Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu, sitawateseni tena zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Hili ndilo asemalo bwana: “Ingawa wana muungano nao ni wengi sana, watakatiliwa mbali na kuangamia. Ingawa nimekutesa wewe, ee Yuda, sitakutesa tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.

Tazama sura Nakili




Nahumu 1:12
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia moja themanini na tano elfu. Na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.


Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.


Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.


Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, atatuma maradhi ya kukondesha kwa wapiganaji walionenepa; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto.


Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.


Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.


Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.


Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Katika siku hiyo Bwana atanyoa kichwa na malaika ya miguuni, kwa wembe ulioajiriwa pande za ng'ambo ya Mto, yaani, kwa mfalme wa Ashuru, nao utaziondoa ndevu pia.


naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hadi shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.


Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.


BWANA akajibu, akawaambia watu wake; Tazameni, nitawaletea nafaka, na divai, na mafuta, nanyi mtashiba kwa vitu hivyo; wala sitawafanya tena kuwa aibu kati ya mataifa;


Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.


Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala joto iliyo yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo