Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 1:11 - Swahili Revised Union Version

11 Ametoka mmoja kwako, akusudiaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungu aliyefanya njama za ulaghai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungu aliyefanya njama za ulaghai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungu aliyefanya njama za ulaghai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga njama dhidi ya Mwenyezi Mungu na kushauri uovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ee Ninawi, kutoka kwako amejitokeza mmoja, ambaye anapanga shauri baya dhidi ya bwana na kushauri uovu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Ametoka mmoja kwako, akusudiaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

Tazama sura Nakili




Nahumu 1:11
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.


Wala Hezekia asiwatumainishe katika BWANA, akisema, Hakika BWANA atatuokoa, wala mji huu hautatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.


Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.


Akaniambia, Mwanadamu, hawa ndio watu wale watungao uovu, na kutoa mashauri mabaya ndani ya mji huu;


Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.


Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.


Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo