Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Amosi 5:16 - Swahili Revised Union Version

16 Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maombolezo katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi, naam, Mwenyezi-Mungu asema: “Patakuwa na kilio kila mahali mitaani; watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’ Wakulima wataitwa waje kuomboleza, na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa hiyo hili ndilo Bwana, yeye Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asemalo: “Kutakuwa na maombolezo barabarani zote, na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa hiyo hili ndilo Bwana, bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote na vilio vya uchungu katika njia kuu zote. Wakulima wataitwa kuja kulia, na waombolezaji waje kuomboleza.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Kwa ajili ya hayo, asema BWANA, Mungu wa majeshi, aliye Bwana; Kutakuwako maomboleza katika njia kuu zote; nao watasema katika njia zote, Ole! Ole! Nao watamwita mkulima aje kuombolea, na hao walio hodari wa kulia waje kuomboleza.

Tazama sura Nakili




Amosi 5:16
23 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.


Maana kilio hicho kimezunguka mipaka ya Moabu, malalamiko yao yamefika hata Eglaimu, na malalamiko yao hata Beer-Elimu.


Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia;


Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.


Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.


Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hakuna apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao.


Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa.


Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa porini na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataangamizwa.


Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea.


Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,


Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.


Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia Kwa ajili ya mume wa ujana wake.


Sikieni, mkashuhudu juu ya nyumba ya Yakobo, asema Bwana, MUNGU wa majeshi.


Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.


Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.


Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila mahali wataitupa, wakinyamaza kimya.


Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia, Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi; Nitaomboleza kama mbweha, Na kulia kama mbuni.


Siku hiyo watatunga mithali juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema, Sisi tumeangamizwa kabisa; Yeye analibadili fungu la watu wangu; Jinsi anavyoniondolea hilo! Awagawia waasi mashamba yetu.


wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.


Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo