Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Amosi 3:3 - Swahili Revised Union Version Je! Watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, watu wawili huanza safari pamoja, bila ya kufanya mpango pamoja kwanza? Biblia Habari Njema - BHND Je, watu wawili huanza safari pamoja, bila ya kufanya mpango pamoja kwanza? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, watu wawili huanza safari pamoja, bila ya kufanya mpango pamoja kwanza? Neno: Bibilia Takatifu Je, watu wawili hutembea pamoja wasipokubaliana kufanya hivyo? Neno: Maandiko Matakatifu Je, watu wawili hutembea pamoja wasipokubaliana kufanya hivyo? BIBLIA KISWAHILI Je! Watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? |
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote.
Je! Simba atanguruma mwituni, asipokuwa na mawindo? Mwanasimba atalia pangoni mwake, ikiwa hakupata kitu?
Lisikieni neno hili, enyi ng'ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.