kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Amosi 1:10 - Swahili Revised Union Version lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Tiro, nao utayateketeza majumba yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro, na kuziteketeza kabisa ngome zake.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro, na kuziteketeza kabisa ngome zake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nitazishushia moto kuta za mji wa Tiro, na kuziteketeza kabisa ngome zake.” Neno: Bibilia Takatifu Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro ambao utateketeza ngome zake.” Neno: Maandiko Matakatifu Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro ambao utateketeza ngome zake.” BIBLIA KISWAHILI lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Tiro, nao utayateketeza majumba yake. |
kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
Nao wataufanya utajiri wako kuwa mateka, na bidhaa yako kuwa mawindo; nao watazibomoa kuta zako, na kuziharibu nyumba zako zipendezazo; nao watatupa mawe yako, na miti yako, na mavumbi yako, kati ya maji.
Nao wataziharibu kuta za Tiro, na kuibomoa minara yake; tena nitakwangua hata mavumbi yake yamtoke, na kumfanya kuwa jabali tupu.
Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
Naam, na ninyi ni kitu gani kwangu, enyi Tiro, na Sidoni, na nchi zote za Filisti? Je! Mtanirudishia malipo? Au mtanitenda neno lolote? Upesi na kwa haraka nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.
lakini nitatuma moto uingie katika nyumba ya Hazaeli, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.
Tazama, Bwana atamwondolea mali zake, naye ataupiga uwezo wake alio nao baharini, naye mwenyewe atateketezwa kwa moto.