Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
2 Yohana 1:12 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike. Biblia Habari Njema - BHND Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ninayo mengi ya kuwaambieni, lakini sipendi kufanya hivyo kwa karatasi na wino; badala yake, natumaini kuwatembeleeni na kuzungumza nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ikamilike. Neno: Bibilia Takatifu Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu. Neno: Maandiko Matakatifu Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa. |
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.
Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
wakati wowote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana natarajia kuwaona ninyi nikiwa katika safari, na kusafirishwa nanyi, baada ya kukaa kwenu kwa muda.
Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana natumaini ya kwamba kwa maombi yenu nitarejeshwa kwenu.
Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.
Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.