Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




2 Samueli 7:5 - Swahili Revised Union Version

Nenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Je, wewe utanijengea nyumba ya kukaa?

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Je, wewe utanijengea nyumba ya kukaa?

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Je, wewe utanijengea nyumba ya kukaa?

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Je, ewe ndiwe wa kunijengea mimi nyumba ili nikae ndani yake?

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo bwana: Je, ewe ndiwe wa kunijengea mimi nyumba ili nikae ndani yake?

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?

Tazama sura
Tafsiri zingine



2 Samueli 7:5
11 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa usiku uo huo, neno la BWANA likamfikia Nathani kusema,


Mfalme akaamuru, nao wakaleta mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa.


Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako.


Nenda, kamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Wewe hutanijengea nyumba ya kukaa;


Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu.


Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.


BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?