Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akasafiri katika nchi yote ya Misri.
2 Samueli 5:4 - Swahili Revised Union Version Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, akatawala miaka arubaini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka arubaini. Biblia Habari Njema - BHND Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka arubaini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka arubaini. Neno: Bibilia Takatifu Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli kwa miaka arobaini. Neno: Maandiko Matakatifu Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. BIBLIA KISWAHILI Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, akatawala miaka arobaini. |
Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akasafiri katika nchi yote ya Misri.
Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arubaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa koo za mababa. Katika mwaka arubaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao wanaume mashujaa.
Na wakati aliotawala juu ya Israeli, ulikuwa miaka arubaini; miaka saba alitawala Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akatawala Yerusalemu.
Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akatawala miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi hata umri wa miaka hamsini, wote waingiao katika utumishi huo, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania.
Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,