Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.
2 Samueli 22:34 - Swahili Revised Union Version Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Biblia Habari Njema - BHND Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Neno: Bibilia Takatifu Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. Neno: Maandiko Matakatifu Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. BIBLIA KISWAHILI Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. |
Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.
Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo, Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.
MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.