Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
2 Samueli 22:27 - Swahili Revised Union Version Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu, lakini mkatili kwa watu walio waovu. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu, lakini mkatili kwa watu walio waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu, lakini mkatili kwa watu walio waovu. Neno: Bibilia Takatifu kwa aliye mtakatifu unajionesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionesha kuwa mkaidi. Neno: Maandiko Matakatifu kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi. BIBLIA KISWAHILI Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi. |
Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.
Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.
Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unatengeneza nini? Au chombo ulichotengeneza hakina mikono?
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.