na hao watu wote nitawarejesha kwako; kama bibi arusi anavyorudi nyumbani kwa mumewe. Kurudi kwa yule mtu umtafutaye ni kana kurudi kwa wote; maana watu wote watakuwa katika amani.
2 Samueli 17:4 - Swahili Revised Union Version Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shauri hilo la Ahithofeli lilimpendeza Absalomu na wazee wote wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Shauri hilo la Ahithofeli lilimpendeza Absalomu na wazee wote wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shauri hilo la Ahithofeli lilimpendeza Absalomu na wazee wote wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Mpango huu ulionekana mzuri kwa Absalomu na kwa wazee wote wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Mpango huu ulionekana mzuri kwa Absalomu na kwa wazee wote wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli. |
na hao watu wote nitawarejesha kwako; kama bibi arusi anavyorudi nyumbani kwa mumewe. Kurudi kwa yule mtu umtafutaye ni kana kurudi kwa wote; maana watu wote watakuwa katika amani.
Ndipo Absalomu akasema, Basi, mwiteni Hushai, Mwarki, naye, tukasikie atakayosema yeye pia.
Basi neno hili likawapendeza mfalme na wakuu wake; naye mfalme akafanya kama alivyopendekeza Memukani.
Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.