Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Samueli 15:15 - Swahili Revised Union Version

Hao watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme, Angalia, sisi watumishi wako tu tayari kutenda lolote atakalolichagua bwana wetu mfalme.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Lakini watumishi wake wakamwambia, “Sisi watumishi wako, bwana wetu mfalme, tuko tayari kufanya lolote unaloamua.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Lakini watumishi wake wakamwambia, “Sisi watumishi wako, bwana wetu mfalme, tuko tayari kufanya lolote unaloamua.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Lakini watumishi wake wakamwambia, “Sisi watumishi wako, bwana wetu mfalme, tuko tayari kufanya lolote unaloamua.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Maafisa wa mfalme wakamjibu, “Watumishi wako tu tayari kufanya lolote mfalme bwana wetu analochagua.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Maafisa wa mfalme wakamjibu, “Watumishi wako tu tayari kufanya lolote mfalme bwana wetu analochagua.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hao watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme, Angalia, sisi watumishi wako tu tayari kutenda lolote atakalolichagua bwana wetu mfalme.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Samueli 15:15
8 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga.

Basi mfalme akatoka na watu wa nyumbani mwake wote wakafuatana naye. Mfalme akaacha wanawake kumi, masuria, ili kuitunza nyumba.

Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumishi wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kuhusu Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme.

Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.

Naye huyo mbebaji silaha akamjibu, Fanya yote yaliyomo moyoni mwako; angalia, mimi hapa ni pamoja nawe, moyo wangu ni kama moyo wako.