1 Wakorintho 4:11 - Swahili Revised Union Version Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tuko uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi. Biblia Habari Njema - BHND Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi. Neno: Bibilia Takatifu Hadi saa hii tuna njaa na kiu, tu uchi, tumepigwa na hatuna makao. Neno: Maandiko Matakatifu Mpaka saa hii tuna njaa na kiu, tu uchi, tumepigwa na hatuna makao. BIBLIA KISWAHILI Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tuko uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; |
Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Lakini Wayahudi wakafika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hata wakampiga kwa mawe Paulo, wakamburuta nje ya mji, wakidhania ya kuwa amekwisha kufa.
Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.
Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yoyote, na katika mambo yoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.