Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Wafalme 15:12 - Swahili Revised Union Version

Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Aliwafukuza nchini wale wafiraji wa kidini, akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wamezitengeneza.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Aliwafukuza nchini wale wafiraji wa kidini, akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wamezitengeneza.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Aliwafukuza nchini wale wafiraji wa kidini, akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wamezitengeneza.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Akawafukuza mahanithi wa mahali pa ibada za sanamu kutoka nchi, na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Akawafukuza mahanithi wa mahali pa kuabudia miungu kutoka nchi na kuondoa sanamu zote ambazo baba zake walikuwa wametengeneza.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Wafalme 15:12
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye.


Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)


Tena mahanithi waliosalia, hao waliosalia siku za Asa baba yake, akawaondoa katika nchi.


Wala hapakuwa na mfalme katika Edomu; naibu alikuwa ndiye mfalme.


Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa BWANA, wanawake walipofuma mapazia ya Ashera.


Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.


Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;


Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.