Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo nchini; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
1 Timotheo 4:5 - Swahili Revised Union Version kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu. Biblia Habari Njema - BHND kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu. Neno: Bibilia Takatifu kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. Neno: Maandiko Matakatifu kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mwenyezi Mungu na kwa kuomba. BIBLIA KISWAHILI kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. |
Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo nchini; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.