Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 7:10 - Swahili Revised Union Version

Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Samueli alipokuwa anatoa ile sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti walikaribia kuwashambulia Waisraeli. Lakini Mwenyezi-Mungu akatoa sauti kubwa ya ngurumo dhidi ya Wafilisti, na kuwavuruga Wafilisti, nao wakatimuliwa mbele ya Waisraeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Samueli alipokuwa anatoa ile sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti walikaribia kuwashambulia Waisraeli. Lakini Mwenyezi-Mungu akatoa sauti kubwa ya ngurumo dhidi ya Wafilisti, na kuwavuruga Wafilisti, nao wakatimuliwa mbele ya Waisraeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Samueli alipokuwa anatoa ile sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti walikaribia kuwashambulia Waisraeli. Lakini Mwenyezi-Mungu akatoa sauti kubwa ya ngurumo dhidi ya Wafilisti, na kuwavuruga Wafilisti, nao wakatimuliwa mbele ya Waisraeli.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile Mwenyezi Mungu alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka hivi kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile bwana alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka hivi kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hata Samweli alipokuwa akiitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na Israeli; lakini BWANA akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile, akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 7:10
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.

Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji; Mungu wa utukufu apiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.

Sauti ya BWANA ina nguvu; Sauti ya BWANA ina utukufu;

Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele.

Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.

BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

BWANA naye akawatapanya mbele ya Israeli, naye Israeli akawaua uuaji ulio mkuu hapo Gibeoni, akawafukuza waikimbilie hiyo njia ya kukwelea kwenda Beth-horoni, na kuwapiga hadi kufikia Azeka, tena hadi kufikia Makeda.

BWANA akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu.

Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.

Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?

Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme.

Kukawa na tetemeko katika kambi, na katika mashamba, na katikati ya watu wote; watu wa ngomeni, na watekaji nyara, wakatetemeka nao; hata na nchi ikatetemeka pia; basi kulikuwa na tetemeko kubwa mno.

Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu dunia yote; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.

Nao watu wa Israeli wakatoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti, wakawapiga, hadi walipofika chini ya Beth-kari.