Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 5:8 - Swahili Revised Union Version

8 Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Walijichagulia miungu mipya, kukawa na vita katika nchi. Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngao kati ya watu 40,000 wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Walijichagulia miungu mipya, kukawa na vita katika nchi. Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngao kati ya watu 40,000 wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Walijichagulia miungu mipya, kukawa na vita katika nchi. Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngao kati ya watu 40,000 wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mungu alichagua viongozi wapya vita vilipokuja malangoni ya mji; lakini hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa watu elfu arobaini katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Walipochagua miungu migeni, vita vilikuja katika malango ya mji, hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 5:8
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;


Wakamwacha BWANA, Mungu wa baba zao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri, wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote, wakajiinamisha mbele yao; wakamkasirisha BWANA, akaghadhibika.


Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za BWANA bali wao hawakufanya hivyo.


Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita; naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.


Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji, Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA; Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli. Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.


Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo