nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hatukulitilia maanani katika siku za Sauli.
1 Samueli 7:1 - Swahili Revised Union Version Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalipeleka ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo. Neno: Bibilia Takatifu Kisha wanaume wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la Mwenyezi Mungu. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu kilimani, na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha watu wa Kiriath-Yearimu wakaja na kulichukua Sanduku la bwana. Wakalipeleka katika nyumba ya Abinadabu juu kilimani na kumweka Eleazari mwanawe wakfu kulichunga Sanduku la bwana. BIBLIA KISWAHILI Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalipeleka ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA. |
nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hatukulitilia maanani katika siku za Sauli.
Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.
Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na mwisho wake ulikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi.
Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.
Nao wakatuma wajumbe waende kwa wenyeji wa Kiriath-yearimu, kusema, Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; basi shukeni, mkalichukue.
Ikawa, tangu sanduku lipelekwe Kiriath-yearimu, muda mrefu ulipita; maana ulikuwa miaka ishirini; na nyumba yote ya Waisraeli wakamwombolezea BWANA.