Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 9:17 - Swahili Revised Union Version

17 Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Basi, Waisraeli wakafunga safari, baada ya siku ya tatu wakafika katika miji yao. Miji hiyo ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-yearimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Basi, Waisraeli wakafunga safari, baada ya siku ya tatu wakafika katika miji yao. Miji hiyo ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-yearimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Basi, Waisraeli wakafunga safari, baada ya siku ya tatu wakafika katika miji yao. Miji hiyo ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-yearimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Ndipo Waisraeli wakasafiri, na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao: yaani Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Ndipo wana wa Israeli wakasafiri na siku ya tatu wakafika kwenye miji yao ya Gibeoni, Kefira, Beerothi na Kiriath-Yearimu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.

Tazama sura Nakili




Yoshua 9:17
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili, viongozi wa vikosi; jina lake mmoja akiitwa Baana, na jina la wa pili Rekabu wana wa Rimoni, Mbeerothi, wa wana wa Benyamini; (kwa maana Beerothi umehesabiwa kuwa wa Benyamini;


na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;


Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;


Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.


Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.


Kwa maana ile maskani ya BWANA, aliyoifanya Musa jangwani, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo mahali pa juu pa Gibeoni.


Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu.


Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu.


Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la BWANA, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia;


ndipo wakaogopa mno, kwa sababu Gibeoni ulikuwa ni mji mkubwa, kama ilivyo miji ya kifalme mmojawapo, tena kwa sababu ulikuwa ni mji mkubwa kupita Ai, tena watu wake wote walikuwa ni mashujaa.


Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu) na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.


kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hadi kufika chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hadi kufika Baala (ndio Kiriath-yearimu);


Kisha mpaka uliendelea na kuzunguka upande wa magharibi wa kuelekea kusini, kutoka huo mlima ulio mkabala wa Beth-horoni upande wa kusini; na mwisho wake ulikuwa hapo Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), ni mji wa wana wa Yuda; huo ndio upande wa magharibi.


Na upande wa kusini ulikuwa ukitoka upande wa mwisho wa Kiriath-yearimu, na mpaka ukatokea upande wa magharibi, ukaendelea hadi chemchemi ya maji, pale Neftoa;


Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya kwamba waliketi kati yao.


Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu.


Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai,


Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako tunatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,


Wakakwea juu na kupiga kambi huko Kiriath-yearimu, katika Yuda; kwa sababu hiyo wakapaita mahali pale jina lake Mahane-dani hata hivi leo; tazama, ni hapo nyuma ya Kiriath-yearimu.


Nao wakatuma wajumbe waende kwa wenyeji wa Kiriath-yearimu, kusema, Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; basi shukeni, mkalichukue.


Na hao watu wa Kiriath-yearimu wakaja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalipeleka ndani ya nyumba ya Abinadabu huko kilimani, nao wakamtenga Eleazari, mwanawe, ili alilinde sanduku la BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo