Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 9:18 - Swahili Revised Union Version

18 Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini Waisraeli hawakuwaua, maana viongozi wa jumuiya ya Israeli walikuwa wamewaapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Hivyo basi, jumuiya yote ikawanungunikia viongozi wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini Waisraeli hawakuwaua, maana viongozi wa jumuiya ya Israeli walikuwa wamewaapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Hivyo basi, jumuiya yote ikawanungunikia viongozi wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini Waisraeli hawakuwaua, maana viongozi wa jumuiya ya Israeli walikuwa wamewaapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli. Hivyo basi, jumuiya yote ikawanung'unikia viongozi wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Kusanyiko lote wakanung’unika dhidi ya hao viongozi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Lakini Waisraeli hawakuwashambulia kwa kuwa viongozi wa kusanyiko walikuwa wamewaapia kwa bwana, Mungu wa Israeli. Kusanyiko lote likanung’unika dhidi ya hao viongozi,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu.

Tazama sura Nakili




Yoshua 9:18
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha BWANA kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli.


Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.


Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.


Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba hukukusudia; kwa nini Mungu akasirishwe na maneno yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?


Mambo yote yawatukia wote sawasawa; kuna tukio moja kwake mwenye haki na kwake asiye haki; kwa mtu mwema na kwa mtu mwovu; kwa mtu aliye safi na kwa mtu asiye safi; kwake yeye atoaye kafara na kwake asiyetoa kafara; kama alivyo huyo mwema ndivyo alivyo mwenye dhambi; yeye aapaye na yeye aogopaye kiapo.


Tena mwanamke atakapomwekea BWANA nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aishi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;


Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.


Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri BWANA, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.


Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako.


Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.


Lakini wakuu wote waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli; basi sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo