Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
1 Samueli 5:12 - Swahili Revised Union Version Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao wale ambao hawakufa walipatwa na majipu hata kilio cha mji kilifika mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Nao wale ambao hawakufa walipatwa na majipu hata kilio cha mji kilifika mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao wale ambao hawakufa walipatwa na majipu hata kilio cha mji kilifika mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Wale ambao hawakufa walipatwa na majipu, na kilio cha mji kilifika hadi mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Wale ambao hawakufa walipatwa na majipu, na kilio cha mji kilikwenda juu hadi mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Na wale wasiokufa walipigwa kwa yale majipu; na kilio cha mji kikafika mbinguni. |
Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua.
Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.
Yuda huomboleza, Na malango yake yamelegea; Wameketi chini wamevaa kaniki; Na kilio cha Yerusalemu kimepaa juu.
Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikia.