Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
1 Samueli 30:27 - Swahili Revised Union Version yaani, kwa hao wa Betheli, na kwa hao wa Ramoth-Negebu, na kwa hao wa Yatiri; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zawadi hizo zilikuwa kwa ajili ya wakazi wa Betheli, wakazi wa Ramothi katika Negebu, wakazi wa Yatiri, Biblia Habari Njema - BHND Zawadi hizo zilikuwa kwa ajili ya wakazi wa Betheli, wakazi wa Ramothi katika Negebu, wakazi wa Yatiri, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zawadi hizo zilikuwa kwa ajili ya wakazi wa Betheli, wakazi wa Ramothi katika Negebu, wakazi wa Yatiri, Neno: Bibilia Takatifu Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri; Neno: Maandiko Matakatifu Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri; BIBLIA KISWAHILI yaani, kwa hao wa Betheli, na kwa hao wa Ramoth-Negebu, na kwa hao wa Yatiri; |
Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Sehemu waliopewa wana wa Yusufu ilianza kutoka mto wa Yordani hapo Yeriko, hapo penye maji ya Yeriko upande wa mashariki, maana, ni hiyo nyika, kukwea kutoka Yeriko kati ya hiyo nchi ya vilima mpaka Betheli;
kisha ikatoka huko Betheli kwendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi;
tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kotekote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila la wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.
Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Beth-aveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai.
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.