Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
1 Samueli 3:4 - Swahili Revised Union Version basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwita Samueli! Naye Samueli, akaitika, “Naam!” Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwita Samueli! Naye Samueli, akaitika, “Naam!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwita Samueli! Naye Samueli, akaitika, “Naam!” Neno: Bibilia Takatifu Kisha Mwenyezi Mungu akamwita Samweli. Samweli akajibu, “Mimi hapa.” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha bwana akamwita Samweli. Samweli akajibu, “Mimi hapa.” BIBLIA KISWAHILI basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. |
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu! Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;
BWANA alipoona ya kuwa ameenda ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kichaka, akasema, Musa! Musa! Akaitika, Mimi hapa.
Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.
Na Mungu ameweka wengine katika kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, aina za usaidizi, maongozi na aina za lugha.
Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.