Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 24:4 - Swahili Revised Union Version

Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Watu wa Daudi wakamwambia, “Ile siku aliyokuambia Mwenyezi-Mungu kuwa atakuja kumtia adui yako mikononi mwako nawe umtendee utakavyoona inafaa, leo imefika.” Ndipo Daudi alipomwendea Shauli polepole kutoka nyuma, akakata pindo la vazi lake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Watu wa Daudi wakamwambia, “Ile siku aliyokuambia Mwenyezi-Mungu kuwa atakuja kumtia adui yako mikononi mwako nawe umtendee utakavyoona inafaa, leo imefika.” Ndipo Daudi alipomwendea Shauli polepole kutoka nyuma, akakata pindo la vazi lake.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Watu wa Daudi wakamwambia, “Ile siku aliyokuambia Mwenyezi-Mungu kuwa atakuja kumtia adui yako mikononi mwako nawe umtendee utakavyoona inafaa, leo imefika.” Ndipo Daudi alipomwendea Shauli polepole kutoka nyuma, akakata pindo la vazi lake.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena Mwenyezi Mungu akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’ ” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena bwana akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’ ” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 24:4
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.

Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?

Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonesha mahali atakapopakimbilia.

Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko.

Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa makamu wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.

Kisha Sauli aliambiwa ya kwamba Daudi amefika Keila. Sauli akasema, Mungu amemtia mkononi mwangu; kwa maana amefungwa ndani, kwa vile alivyoingia katika mji wenye malango na makomeo.

Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.

BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.