Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 24:10 - Swahili Revised Union Version

10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Sasa tazama, leo umejionea kwa macho yako mwenyewe; ulipokuwa pangoni Mwenyezi-Mungu alikutia mikononi mwangu. Baadhi ya watu wangu waliniambia nikuue, lakini nilikuhurumia. Nikasema sitanyosha mkono wangu dhidi ya bwana wangu kwani yeye ameteuliwa na Mwenyezi-Mungu kwa kupakwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Sasa tazama, leo umejionea kwa macho yako mwenyewe; ulipokuwa pangoni Mwenyezi-Mungu alikutia mikononi mwangu. Baadhi ya watu wangu waliniambia nikuue, lakini nilikuhurumia. Nikasema sitanyosha mkono wangu dhidi ya bwana wangu kwani yeye ameteuliwa na Mwenyezi-Mungu kwa kupakwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi Mwenyezi Mungu alivyokutia mikononi mwangu huko pangoni. Watu wengine walisisitiza nikuue, lakini nilikuacha, nikisema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa sababu yeye ni mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi bwana alivyokutia mikononi mwangu huko pangoni. Watu wengine walisisitiza nikuue, lakini nilikuacha, nikisema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa sababu yeye ni mpakwa mafuta wa bwana.’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 24:10
10 Marejeleo ya Msalaba  

Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.

Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu.

BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya, Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,

Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonesha mahali atakapopakimbilia.

Wasingiziaji wamekuwamo ndani yako, ili kumwaga damu; na ndani yako wamekula juu ya milima; kati yako wamefanya uasherati.

Usiende huku na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usijifaidi kwa damu ya jirani yako; mimi ndimi BWANA.

Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.

Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo