Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 24:18 - Swahili Revised Union Version

18 Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Leo, umeonesha jinsi ulivyo mwema kwangu. Hukuniua ijapokuwa Mwenyezi-Mungu alinitia mikononi mwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Leo, umeonesha jinsi ulivyo mwema kwangu. Hukuniua ijapokuwa Mwenyezi-Mungu alinitia mikononi mwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Leo, umeonesha jinsi ulivyo mwema kwangu. Hukuniua ijapokuwa Mwenyezi-Mungu alinitia mikononi mwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Sasa umeniambia kuhusu mema uliyonitendea. Mwenyezi Mungu alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Sasa umeniambia juu ya mema uliyonitendea. bwana alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Nawe umeonesha leo jinsi ulivyonitendea mema, kwani BWANA aliponitia mikononi mwako, hukuniua.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 24:18
10 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.


Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha mahali penye usalama.


Basi adui na anifuatie, Na kuikamata nafsi yangu; Naam, aukanyage uzima wangu, Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.


Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu.


Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? BWANA akasema, Watakutia.


Kisha Sauli aliambiwa ya kwamba Daudi amefika Keila. Sauli akasema, Mungu amemtia mkononi mwangu; kwa maana amefungwa ndani, kwa vile alivyoingia katika mji wenye malango na makomeo.


Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi BWANA alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.


Maana mtu akimwona adui yake, je! Atamwacha aende zake salama? Basi BWANA na akulipe mema kwa haya uliyonitendea leo.


BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.


Ndipo Abishai akamwambia Daudi, Mungu amemtia adui yako mikononi mwako leo; basi, niache nimpige kwa hilo fumo hadi chini kwa pigo moja, sitampiga mara ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo