Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya Israeli.
1 Samueli 2:7 - Swahili Revised Union Version BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini, na baadhi wawe matajiri. Wengine huwashusha, na wengine huwakweza. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini, na baadhi wawe matajiri. Wengine huwashusha, na wengine huwakweza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini, na baadhi wawe matajiri. Wengine huwashusha, na wengine huwakweza. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza. Neno: Maandiko Matakatifu bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza. BIBLIA KISWAHILI BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. |
Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya Israeli.
Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.
Naye Hezekia akawa na mali nyingi mno na heshima; akajitengenezea hazina za fedha, za dhahabu, za vito, za manukato, za ngao, na za namna zote za vyombo vya thamani;
Tena akajitengenezea miji, na mali za kondoo na ng'ombe kwa wingi; maana Mungu alimtajirisha sana sana.
akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
Kwa maana kutakuwa siku ya BWANA wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.
Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.