Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
1 Samueli 15:7 - Swahili Revised Union Version Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shauli aliwashinda Waamaleki kuanzia Havila hadi Shuri, mashariki ya Misri. Biblia Habari Njema - BHND Shauli aliwashinda Waamaleki kuanzia Havila hadi Shuri, mashariki ya Misri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shauli aliwashinda Waamaleki kuanzia Havila hadi Shuri, mashariki ya Misri. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Sauli akawashambulia Waamaleki toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Sauli akawashambulia Waamaleki toka Havila mpaka Shuri, hadi mashariki ya Misri. BIBLIA KISWAHILI Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri. |
Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.
Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
lakini haitakuwa heri kwa mwovu, wala hatazidisha siku zake, zilizo kama kivuli; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.
Naye kwa ushujaa, akawapiga Waamaleki, na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa mikono ya waliowateka nyara.
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, mpaka nchi ya Misri.
Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;