Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Zekaria 7:7 - Swahili Revised Union Version

7 Je, Hayo siyo maneno aliyoyasema BWANA kwa vinywa vya manabii wa zamani, wakati Yerusalemu ulipokaliwa na watu na kufanikiwa, na miji yake iliyokuwa ikiuzunguka; na wakati ule ambao nchi ya Negebu na Shefela ilipokuwa ikikaliwa na watu?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Haya ndiyo mambo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliwaambieni kupitia kwa manabii wa hapo kwanza, wakati mji wa Yerusalemu ulikuwa umestawi na wenye wakazi tele, na wakati ambapo kulikuwa na wakazi wengi katika miji ya kandokando yake na katika eneo la Negebu na nyanda za Shefela.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Haya ndiyo mambo ambayo mimi Mwenyezi-Mungu niliwaambieni kupitia kwa manabii wa hapo kwanza, wakati mji wa Yerusalemu ulikuwa umestawi na wenye wakazi tele, na wakati ambapo kulikuwa na wakazi wengi katika miji ya kandokando yake na katika eneo la Negebu na nyanda za Shefela.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Je, haya sio maneno ya Mwenyezi Mungu aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefela zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Je, haya sio maneno ya bwana aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Je, Hayo siyo maneno aliyoyasema BWANA kwa vinywa vya manabii wa zamani, wakati Yerusalemu ulipokaliwa na watu na kufanikiwa, na miji yake iliyokuwa ikiuzunguka; na wakati ule ambao nchi ya Negebu na Shefela ilipokuwa ikikaliwa na watu?

Tazama sura Nakili

Zekaria 7:7
23 Marejeleo ya Msalaba  

Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

Miji ya Negebu imefungwa malango yake, wala hapana mtu wa kuyafungua; Yuda amechukuliwa mateka; amechukuliwa kabisa mateka.

Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, na milima, na upande wa Negebu, wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA

Mimi nilisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutoitii sauti yangu.

Watu watanunua mashamba kwa fedha, watazitia sahihi hati zake, na kuzipiga mhuri, na kuwaita mashahidi, katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, na katika miji ya nchi yenye vilima, na katika miji ya nchi tambarare, na katika miji ya Negebu; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, asema BWANA.

Katika miji ya nchi ya vilima, katika miji ya nchi tambarare, katika miji ya Negebu, na katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo karibu na Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mikono yake anayewahesabu, asema BWANA.

Tena nilituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linalochukiza.

lakini niliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.

Maana kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu; kama mkihukumu hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake;

Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na maneno ya BWANA wa majeshi, aliyoyatuma kwa roho yake, kwa mkono wa manabii wa kwanza; kwa sababu hiyo ghadhabu kuu ikatoka kwa BWANA wa majeshi.

Na wakati mnapokula chakula na kunywa, je, Hamli kwa ajili ya nafsi zenu, na kunywa kwa ajili ya nafsi zenu?

Kisha neno la BWANA likamjia Zekaria, kusema,

na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo