Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 1:7 - Swahili Revised Union Version

7 Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Usiseme kwamba wewe ni kijana bado. Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao, na yote nitakayokuamuru utayasema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Usiseme kwamba wewe ni kijana bado. Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao, na yote nitakayokuamuru utayasema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Usiseme kwamba wewe ni kijana bado. Utakwenda kwa watu wote nitakaokutuma kwao, na yote nitakayokuamuru utayasema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini Mwenyezi Mungu akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini bwana akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.

Tazama sura Nakili




Yeremia 1:7
20 Marejeleo ya Msalaba  

Mikaya akasema, Kama BWANA aishivyo, neno lile BWANA aniambialo, ndilo nitakalolinena.


Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.


Mikaya akasema, Kama aishivyo BWANA, neno lile atakalolinena Mungu wangu, ndilo nitakalolinena.


BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo.


BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.


Ikawa Yeremia alipokwisha kuwaambia watu wote maneno yote ya BWANA, Mungu wao, ambayo BWANA, Mungu wao, amemtuma kwao, yaani, maneno hayo yote,


Nawe utawaambia maneno hayo yote; lakini hawatakusikiliza, nawe utawaita; lakini hawatakuitikia.


Nawe utawaambia maneno yangu, iwe watasikia au hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.


Lakini hapo nitakaposema nawe, nitafumbua kinywa chako, nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. Yeye asikiaye na asikie; naye akataaye na akatae; maana wao ni nyumba yenye kuasi.


naye BWANA akanitwaa, katika kufuatana na kundi; BWANA akaniambia, Nenda uwatabirie watu wangu Israeli.


Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.


Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.


Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wowote kusema neno lolote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo