Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yakobo 3:8 - Swahili Revised Union Version

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini hakuna mtu aliyefaulu kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini hakuna mtu aliyefaulu kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini hakuna mtu aliyefaulu kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Tazama sura Nakili

Yakobo 3:8
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wamenoa ndimi zao na kuwa kama za nyoka, Na katika midomo yao mna sumu ya fira.

Kinywa chake ni laini kuliko siagi, Bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, Lakini yanakata kama upanga mkali.

Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.

Wana sumu mfano wa sumu ya nyoka; Wao ni kama fira kiziwi azibaye sikio lake.

Tazama, kwa vinywa vyao huteuka, Midomoni mwao mna panga, Kwa maana ni nani asikiaye?

Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema; Na mwenye ulimi wa upotovu huanguka katika misiba.

Nyoka akiuma kabla hajachezeshwa, Basi hakuna faida ya mchezeshaji.

Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira iko chini ya midomo yao.

Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka.

Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfululizo wa maumbile, nao huwashwa moto na Jehanamu.

Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

Lile joka kuu likatupwa, yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika wake wakatupwa pamoja naye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo