Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 3:2 - Swahili Revised Union Version

2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mlangoni mwa hema la mkutano. Hao makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mlangoni mwa hema la mkutano. Hao makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mlangoni mwa hema la mkutano. Hao makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani, wana wa Haruni, watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Haruni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.

Tazama sura Nakili




Walawi 3:2
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha utamleta huyo ng'ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng'ombe.


Kisha utamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania.


Pia mtwae kondoo dume mmoja; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo dume.


Kisha utamchinja huyo kondoo dume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kandokando.


Kisha mtwae huyo kondoo wa pili; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.


Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.


Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.


Mtu yeyote wa nyumba ya Israeli atakayechinja ng'ombe, mwana-kondoo, au mbuzi, ndani au nje ya kambi,


wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, kama matoleo kwa BWANA mbele ya hema ya BWANA; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na atatupiliwa mbali na watu wake;


Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa BWANA itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,


Na kuweka mkono wako katika kichwa cha mwana-kondoo yule, atachinjwa mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.


Kisha akamsongeza kondoo dume wa pili, huyo kondoo wa kuwaweka wakfu; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.


Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimdunga; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.


Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, iwe harufu ya kupendeza.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake.


Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.


Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo