Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 3:3 - Swahili Revised Union Version

3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa BWANA itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mafuta yote yanayofunika na yaliyo juu ya matumbo ya mnyama wa sadaka hiyo ya amani atayateketeza kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mafuta yote yanayofunika na yaliyo juu ya matumbo ya mnyama wa sadaka hiyo ya amani atayateketeza kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mafuta yote yanayofunika na yaliyo juu ya matumbo ya mnyama wa sadaka hiyo ya amani atayateketeza kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Katika hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: sehemu za ndani na mafuta yote yanayoungana nazo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa BWANA itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,

Tazama sura Nakili




Walawi 3:3
25 Marejeleo ya Msalaba  

Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Lakini mimi nimeifurahia sheria yako.


Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.


Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo dume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kulia; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;


Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.


Zifanye akili za watu hawa zipumbae, na uyatie uzito masikio yao, na uyafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.


Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.


Lakini makuhani Walawi, wana wa Sadoki, waliosimamia patakatifu pangu, hapo wana wa Israeli walipopotea na kuniacha, hao ndio watakaonikaribia ili kunihudumia; nao watasimama mbele zangu, kunitolea mafuta na damu, asema Bwana MUNGU;


Kisha atamkata vipande vyake, pamoja na kichwa chake, na mafuta yake; kisha atavipanga vile vipande juu ya kuni zilizo juu ya madhabahu;


kisha wana wa Haruni, makuhani, watazipanga kuni zilizo juu ya moto uliopo juu ya madhabahu;


Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu.


Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.


na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na hicho kitambi kilicho katika ini, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa.


vile vile kama yanavyoondolewa katika ng'ombe wa kuchinjwa kwa sadaka za amani; kisha huyo kuhani atayateketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.


mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atavileta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA.


na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kuwa dhabihu kwa BWANA kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia.


lakini mafuta, na figo, na kitambi kilichotoka katika ini ya hiyo sadaka ya dhambi, akaviteketeza juu ya madhabahu, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia.


Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.


na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.


mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.


Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, huja mtumishi wa kuhani, akamwambia yule mwenye kuitoa dhabihu, Mtolee kuhani nyama ya kuoka; kwa kuwa hataki kupewa nyama iliyotokoswa, bali nyama mbichi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo