Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 3:1 - Swahili Revised Union Version

1 Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “ ‘Ikiwa mtu anatoa sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Na matoleo yake kwamba ni sadaka za amani; kwamba asongeza katika ng'ombe, dume au jike, atamtoa huyo asiye na dosari mbele za BWANA.

Tazama sura Nakili




Walawi 3:1
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.


Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.


akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng'ombe.


navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya BWANA.


Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;


Nao watakapozitimiza siku hizo, itakuwa, siku ya nane na baadaye, makuhani watatoa sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu, na sadaka zenu za amani nami nitawakubali ninyi, asema Bwana MUNGU.


na mwana-kondoo mmoja wa kundi katika mia mbili, katika malisho ya Israeli yenye maji; kwa sadaka ya unga, na kwa sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka za amani, ili kuwafanyia upatanisho, asema Bwana MUNGU.


Na matoleo yake kwamba ni katika kundi, katika kondoo, au katika mbuzi, kuwa sadaka ya kuteketezwa; atatoa dume asiye na dosari.


Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.


ili wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, wazilete kwa BWANA, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa BWANA.


Na matoleo yake kwa sadaka za amani atakayomchinjia BWANA, kwamba ni katika kundi la kondoo; dume au jike, atamtoa huyo aliye mkamilifu.


Huyo ng'ombe dume naye akamchinja, na huyo kondoo dume pia, dhabihu ya sadaka za amani, zilizokuwa kwa ajili ya watu; na wanawe Haruni wakamsogezea ile damu, naye akainyunyiza katika madhabahu pande zote,


na ng'ombe dume, na kondoo dume, kwa sadaka za amani, ili kuwachinja mbele za BWANA; na sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta; kwa maana, BWANA hivi leo atawatokea.


Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.


Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.


Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee mtawala wako; Je, Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi.


Tena hapo utakapomwandaa ng'ombe dume kwa sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa kuondoa nadhiri, au kwa sadaka za amani kwa BWANA;


naye atasongeza sadaka yake kwa BWANA, mwana-kondoo mmoja dume wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya kuteketezwa, na mwana-kondoo jike mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi, na kondoo dume mmoja asiye na dosari kwa sadaka ya amani,


na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.


tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.


nawe zisongeze sadaka zako za kuteketezwa, nyama na damu, juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako; na damu ya dhabihu zako uimwage juu ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako, na wewe utakula nyama yake.


na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.


na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.


hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Ndipo wana wa Israeli wote, na hao watu wote, wakakwea, wakaenda Betheli, na kulia, wakaketi hapo mbele za BWANA, wakafunga siku hiyo hadi jioni; nao wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Kisha kesho yake, hao watu wakaamka asubuhi na mapema, wakajenga madhabahu huko, wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo