Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 3:11 - Swahili Revised Union Version

11 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kuhani ataviteketeza hivyo vyote juu ya madhabahu kama chakula anachotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Kuhani ataviteketeza hivyo vyote juu ya madhabahu kama chakula anachotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kuhani ataviteketeza hivyo vyote juu ya madhabahu kama chakula anachotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa moto.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.

Tazama sura Nakili




Walawi 3:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.


kuwa mmewaingiza wageni, ambao mioyo yao haikutahiriwa, wala miili yao haikutahiriwa, wawe ndani ya patakatifu pangu, wapatie unajisi, naam, nyumba yangu, mtoapo sadaka ya chakula changu, mafuta na damu; nao wameyavunja maagano yangu, juu ya machukizo yenu yote.


Nena na Haruni, umwambie, Mtu yeyote wa vizazi vyenu vyote aliye na kilema asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.


Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.


Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi BWANA niwatakasaye ninyi ni mtakatifu.


Wala msisongeze chakula cha Mungu wenu katika wanyama hao mmojawapo kitokacho mkononi mwa mgeni; kwa sababu uharibifu wao uko ndani yao, wana kilema ndani yao; hawatakubaliwa kwa ajili yenu.


Naye kuhani atayateketeza kwa moto juu ya madhabahu; ni chakula cha dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, iwe harufu ya kupendeza; mafuta yote ni ya BWANA.


Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa.


Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa.


Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao.


Mtasongeza sadaka kwa jinsi hii kila siku kwa muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.


Yeye ambaye hakumhurumia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje pia kutupa chochote kingine pamoja naye?


Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.


Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo