Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nahumu 3:19 - Swahili Revised Union Version

19 Jeraha lako halipunguziki; donda lako haliponyeki; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani aliyewahi kuukwepa ukatili wako usio na mwisho?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako, vidonda vyako ni vya kifo. Wote wanaosikia habari zako wanashangilia. Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako, vidonda vyako ni vya kifo. Wote wanaosikia habari zako wanashangilia. Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hakuna wa kuyapa nafuu majeraha yako, vidonda vyako ni vya kifo. Wote wanaosikia habari zako wanashangilia. Maana ni nani aliyeuepa ukatili wako usio na kikomo?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako; jeraha lako ni la kukuua. Kila anayesikia habari zako, hupiga makofi kwa kuanguka kwako, kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa na ukatili wako usio na mwisho?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako; jeraha lako ni la kukuua. Kila anayesikia habari zako, hupiga makofi kwa kuanguka kwako, kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa na ukatili wako usio na mwisho?

Tazama sura Nakili

Nahumu 3:19
20 Marejeleo ya Msalaba  

Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.

Tazama, umesikia habari ya mambo yote, ambayo wafalme wa Ashuru wamezitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa je! Utaokoka wewe?

Ni kweli, BWANA, wafalme wa Ashuru wameziharibu nchi zote, na mashamba yao,

Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.

Maana BWANA asema hivi, Maumivu yako hayaponyeki, na jeraha lako ni kubwa.

Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.

Hao watu wote wapitao Hukupigia makofi; Humzomea binti Yerusalemu, Na kutikisa vichwa vyao; Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri, Furaha ya dunia yote?

Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako;

Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.

Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.

Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wameleweshwa kwa mvinyo ya uasherati wake.

Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo