Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nahumu 3:15 - Swahili Revised Union Version

15 Huko moto utakuteketeza; Upanga utakukatilia mbali; Utakumeza kama tunutu alavyo; Jifanye kuwa wengi kama tunutu! Jifanye kuwa wengi kama nzige!

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini huko pia moto utawateketezeni, upanga utawakatilia mbali; utawamaliza kama nzige walavyo. Ongezekeni kama nzige, naam, ongezekeni kama panzi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini huko pia moto utawateketezeni, upanga utawakatilia mbali; utawamaliza kama nzige walavyo. Ongezekeni kama nzige, naam, ongezekeni kama panzi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini huko pia moto utawateketezeni, upanga utawakatilia mbali; utawamaliza kama nzige walavyo. Ongezekeni kama nzige, naam, ongezekeni kama panzi!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Huko moto utakuteketeza, huko upanga utakuangusha chini na kama vile panzi, watakumaliza. Ongezeka kama panzi, ongezeka kama nzige!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Huko moto utakuteketeza, huko upanga utakuangusha chini na kama vile panzi, watakumaliza. Ongezeka kama panzi, ongezeka kama nzige!

Tazama sura Nakili

Nahumu 3:15
10 Marejeleo ya Msalaba  

Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.

BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.

Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.

Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.

Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.

Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.

Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako.

Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo