Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nahumu 3:14 - Swahili Revised Union Version

14 Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako; Zitie nguvu ngome zako; Ingia katika udongo, yakanyage matope, Itie nguvu tanuri ya kuokea matofali.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa; imarisheni ngome zenu. Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga, tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa; imarisheni ngome zenu. Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga, tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Tekeni maji muwe tayari kuzingirwa; imarisheni ngome zenu. Pondeni udongo kwa kuukanyagakanyaga, tayarisheni tanuri ya kuchomea matofali!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, imarisha ulinzi wako, Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, yakanyage matope, karabati tanuru la kuchomea matofali!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, imarisha ulinzi wako, Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, yakanyage matope, karabati tanuru la kuchomea matofali!

Tazama sura Nakili

Nahumu 3:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Siye Hezekia anayewashawishi, mtolewe kufa kwa njaa na kwa kiu, akisema, BWANA, Mungu wetu, atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?

Nimechimba na kunywa maji, na kwa nyayo za miguu yangu nitaikausha mito yote ya Misri.

Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.

Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.

Yeye apondaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.

Kwa maana BWANA anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo