Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 43:26 - Swahili Revised Union Version

26 Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka chini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Yosefu, aliporudi nyumbani, wakamletea zile zawadi walizokuwa nazo, wakamwinamia kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Yosefu, aliporudi nyumbani, wakamletea zile zawadi walizokuwa nazo, wakamwinamia kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Yosefu, aliporudi nyumbani, wakamletea zile zawadi walizokuwa nazo, wakamwinamia kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Yusufu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Yusufu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi walizokuwa nazo, ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia hadi nchi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka chini.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 43:26
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Alaaniwe yeyote yule atakayekulaani, Na abarikiwe yeyote yule atakayekubariki.


Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake.


Naye Yusufu alikuwa ni mkuu juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake.


Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.


Wakasema, Mtumishi wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.


Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi.


Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.


Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo