Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 34:7 - Swahili Revised Union Version

7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka malishoni; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, jambo lisilostahili kutendeka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 na wakati huohuo watoto wa kiume wa Yakobo wakawa wanarudi nyumbani kutoka malishoni. Waliposikia hayo, vijana hao wakaona uchungu mwingi na kukasirika sana, kwa vile Shekemu alikuwa amewafanyia watu wa Israeli ovu hilo la kulala na binti ya Yakobo, maana jambo hilo lilikuwa mwiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 na wakati huohuo watoto wa kiume wa Yakobo wakawa wanarudi nyumbani kutoka malishoni. Waliposikia hayo, vijana hao wakaona uchungu mwingi na kukasirika sana, kwa vile Shekemu alikuwa amewafanyia watu wa Israeli ovu hilo la kulala na binti ya Yakobo, maana jambo hilo lilikuwa mwiko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 na wakati huohuo watoto wa kiume wa Yakobo wakawa wanarudi nyumbani kutoka malishoni. Waliposikia hayo, vijana hao wakaona uchungu mwingi na kukasirika sana, kwa vile Shekemu alikuwa amewafanyia watu wa Israeli ovu hilo la kulala na binti ya Yakobo, maana jambo hilo lilikuwa mwiko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Basi wana wa Yakobo wakarudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotukia. Walijawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti Yakobo, jambo ambalo halikupasa kutendwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka malishoni; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, jambo lisilostahili kutendeka.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 34:7
27 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.


Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye.


Hamori akasema nao, akinena, roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe.


Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.


Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana.


Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee BWANA, milele na milele.


Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,


kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.


Na kama mkutano mzima wa Israeli ukifanya dhambi bila kukusudia, na jambo lenyewe likayafichamania macho ya huo mkutano, nao wamefanya mojawapo katika mambo yaliyozuiliwa na BWANA, kwamba wasiyafanye, nao wamepata hatia;


Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu yeyote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lolote ambalo BWANA amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lolote la maneno hayo;


Na mtu yeyote kati ya watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lolote katika hayo ambayo BWANA alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia;


Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu elfu ishirini na tatu.


Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.


Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;


Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;


na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na wanaume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.


Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.


Basi, viueni viungo vyenu vilivyo vya kidunia, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;


Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.


Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.


Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.


Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli.


Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Basi nikamtwaa huyo suria wangu, na kumkata vipande, na kumpeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli; kwa sababu wametenda maovu makuu na upumbavu katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo